Full-Width Version (true/false)


Niyonzima: kupata Namba Simba itakuwa kazi

 

KUFUATIA Simba kuanza kwa kasi kusajili baadhi ya wachezaji waliong'ara Ligi Kuu Tanzania Bara, huku ikitajiwa kushusha nyota  wa kimataifa wa kiwango cha juu, kiungo wa timu hiyo, Haruna Niyonzima, amesema hatua hiyo itafanya ushindani wa namba kuwa mkubwa ndani ya kikosi hicho. 

Akizungumza mjini hapa kabla ya kuanza mazoezi kwenye Uwanja wa Rift Valley jana asubuhi, Niyonzima, alisema wachezaji walioongezwa kwenye timu hiyo ni wazuri na wanauwezo wa kuichezea timu hiyo. “Hii itafanya sasa ushindani wa namba uwe mkubwa sana zaidi ya ule uliokuwapo awali, na hili si jambo baya, litatufanya sisi kama wachezaji kujituma ili kuwashawishi makocha kutupanga,” alisema Niyonzima. 

Akizungumzia michuano ya SportPesa Super Cup inayoendelea mjini hapa, Niyonzima, alisema ni fursa kwao kuonyesha ubora wao hasa kwa wale wachezaji ambao hawakupata nafasi kubwa ya kucheza kwenye michezo ya Ligi Kuu.“Kwa sisi ambao hatukupata nafasi kutokana na kuwa majeruhi au sababu nyingine yoyote, michuano hii itatusaidia sasa kuturudisha kwenye mstari,” alisema Niyonzima. Aidha, alisema mchezo wa leo dhidi ya Kariobang Shark ni muhimu sana kwao kushinda. 

“Hatutaki kuishia hatua ya awali, tunafahamu ili tuweze kusonga mbele tunatakiwa kushinda mchezo wa kesho (leo), kama wachezaji tutapambana kwa nguvu zetu zote kuhakikisha tunapata matokeo mazuri,” alihitimisha.

No comments

Powered by Blogger.