Full-Width Version (true/false)


Niyonzima kuwakosa Gor mahia fainali ya sportpesa super cup, sababu ni hii
Kiungo Mnyarwanda wa klabu ya Simba, Haruna Niyonzima, atakosekana leo katika kikosi chake wakati kikikabiliana na Gor Mahia FC katika fainali ya SportPesa Super Cup.

Kiungo huyo ataukosa mtanange huo kutokana na kuwa na idadi ya kadi mbili za njano ambazo haziruhusu mchezaji kucheza mchezo unaofuata kwa mujibu wa kanuni na taratibu za mashindano hayo.

Niyonzima alipata kadi hizo katika mchezo wa kwanza dhidi ya Kariobang Sharks na uliofuata wa hatua ya nusu fainali dhidi ya Kakamega HomeBoyz FC.

Mchezo huo wa fainali utaanza majira ya saa 9 kamili alasiri ikiwa ni baada ya ule wa kuwania nafasi ya tatu kati ya Kakamega HomeBoyz FC dhidi ya Singida United.
Ikumbukwe mshindi wa taji hilo atajipatia kiasi cha fedha, shilingi milioni 60 pamoja na kupata nafasi ya kucheza na Everton FC, kwenye Uwanja wake wa Goodison Park, England.

No comments

Powered by Blogger.