Full-Width Version (true/false)


Nyota watakaoshudia Kombe la Dunia nyumbani

Kombe la Dunia ni hatua ya juu zaidi ya mafanikio kwa mwanasoka yeyote kwa sababu ni mashindano yanayofanyika mara moja baada ya miaka minne. 

Hata hivyo mashindano haya kuna wachezaji ambao kwa bahati mbaya wameyakosa kwa sababu mbalimbali wengine ikiwa ni majeruhi. 

Alex Oxlade-Chamberlain akiwa katika kiwango cha juu Liverpool, ameachwa katika kikosi cha England kutokana na kuwa majeruhi, pia yupo Laurent Koscielny aliumia akitumikia Arsenal jambo lililomfanya achwe katika kikosi cha Ufaransa. 

Mbali ya hao hawa hapa ni kikosi cha nyota waliokosa fainali za Kombe la Dunia baada ya nchi zao kushindwa kufuzu kwa fainali hizo. 

MakipaGianluigi Buffon (Italia), Jan Oblak (Slovenia), Jasper Cillessen (Uholanzi) Mabeki David Alaba (Austria); Andrea Barzagli, Leonardo Bonucci, Giorgio Chiellini (Italia); Faouzi Ghoulam (Algeria); Antonio Valencia (Ecuador); Virgil Van Dijk (Uholanzi) Viungo Marek Hamsik (Slovakia), Naby Keita (Guinea), Henrikh Mkhitaryan (Armenia), Miralem Pjanic (Bosnia & Herzegovina), Christian Pulisic (USA), Thomas Partey (Ghana), Arturo Vidal (Chile), Wilfried Zaha (Ivory Coast) Washambuliaji Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon), Gareth Bale (Wales), Arjen Robben (Uholanzi), Edin Dzeko (Bosnia & Herzegovina), Alexis Sanchez (Chile) Wengine ni:Gianluigi Donnarumma (Italia), Stefan de Vrij (Uholanzi), Daley Blind (Uholanzi), Eric Bailly (Ivory Coast), Sokratis Papastathopoulos (Ugiriki), Serge Aurier (Ivory Coast), Marco Verratti (Italia), Gary Medel (Chile), Charles Aranguiz (Chile), Hakan Calhanoglu (Uturuki), Aaron Ramsey (Wales), Riyad Mahrez (Algeria), Cenk Tosun (Uturuki), Vincent Aboubakar (Cameroon), Andriy Yarmolenko (Ukraine), Stevan Jovetic (Montenegro), Andrea Belotti (Italia).

No comments

Powered by Blogger.