Full-Width Version (true/false)


Nyuki watibua mechi Copa Umisseta Mwanza.

 Kundi kubwa la nyuki lililolokuwa likipita kwenye viwanja vya Chuo cha Ualimu Butimba lilitibua mechi ya soka kati ya Mbeya na Lindi wasichana katika mashindano ya Copa Umisseta. Wakati nyuki hao wakikatisha uwanjani hapo, jambo lililomfanya mwamuzi wa mchezo huo, Peter Nico wa Morogoro kuwahimiza wachezaji kulala nchini na yeye akalala ili kuwapisha nyuki hao kupita tukio lililochukua dakika tano (5). 

Mchezo huo uliopendelea Mbeya wasichana iliondoka na ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Lindi. Mashabiki waliojitokeza kushuhudia mchezo huo nao walijikuta wakilazimika kulala nchini baada ya kuwaona wachezaji na refarii wamelala bila kujua kinachoendelea kwa sekunde kadhaa hadi kundi hilo la nyuki ambalo lilipita chini usawa wa vimo vya wachezaji.

No comments

Powered by Blogger.