Full-Width Version (true/false)


PAC kukabidhi taarifa ya vigogo BOT leo

 

KAMATI ya Hesabu za Serikali na Mashirika ya Umma (PAC) leo inakabidhi kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai taarifa kuhusu bodi na menejimenti ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT)  inayotuhumiwa kutumia bima binafsi badala ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).
Hatua hiyo inakuja baada ya Jumanne iliyopita, Spika Ndugai kuagiza PAC kuihoji BoT kuhusu tuhuma hizo zilizotolewa na Mbunge wa Ulanga, Gudluck Mlinga (CCM).
Akizungumza   na MTANZANIA jana, Mwenyekiti wa PAC, Naghenjwa Kaboyoka alisema  atakabidhi leo taarifa hiyo kwa Spika kama  alivyoagiza.
“Tayari tumekamilisha kuwahoji BoT, Mlinga na NHIF na kesho (leo) tutakabidhi. Leo nafanya kazi ya kupitia taarifa.
“Kuhusu tulichobaini siwezi kusema chochote kwa sababu hii ni taarifa ya Spika, yeye ndiye ataamua baada ya sisi kukabidhi, aisome au lah,”alisema Kaboyoka.
Akichangia bajeti ya Wizara ya Fedha, Mlinga alisema   fedha za matibabu kwa maofisa wa BoT kwa mwezi ni Sh bilioni 12, lakini wangekuwa wanatumia mfuko wa NHIF matibabu yao kwa mwezi yangekuwa Sh bilioni moja tu.
“Hivi ninavyoongea watumishi wa BoT ndiyo taasisi inayotumia fedha nyingi katika matibabu bila msingi wowote.

No comments

Powered by Blogger.