Full-Width Version (true/false)


Paul Makonda kuwatatumia askari 400 wa operesheni usafi wa mazingira Dar
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema ataanzisha operesheni ya usafi wa mazingira itakayoshirikisha askari wa Jeshi la Kujenga Taifa 400 ili kuhakikisha jiji hilo linakuwa safi tofauti na lilivyo sasa. “Naomba unifikishie salamu hizi kwa Rais John Magufuli tutawakamata, hapa ni askari wa JKT (Jeshi la Kujenga Taifa) 400. 

Ziba masikio nataka niendeshe operesheni ili jiji linyooke na liwe safi," amesema Makonda. Makonda ametoa kauli hiyo leo Jumanne Juni 5 2018 wakati wa maadhimisho ya siku mazingira duniani ambayo kitaifa yamefanyika viwanja vya Mnazi Mmoja na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan. 

Makonda amemweleza Samia kuwa bado usafi katika jiji la Dar es Salaam ni tatizo na kwamba watu ni wachafu na wanatia aibu. "Hapa unawaona ni nadhifu, lakini huko walikotoka hawajaacha mazingira vizuri. Makamu wa Rais naomba uzibe masikio kidogo kwa hii operesheni."

No comments

Powered by Blogger.