Full-Width Version (true/false)


Polisi Tabora yakamata watu 4 wakiwa na Mirungi na Gunia 5 za Bhangi


Akiongea na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora SACP, WILBROD MUTAFUNGWA  amemtaja mtu huyo anayefahamika kwa jina MASHALA SABUNI HAMIS, Miaka 34,  mkazi wa Fumba kata ya Ulyankulu  akiwa na magunia  20 ya  Bhangi pamoja na mbegu za Bhangi magunia 05.
Mtuhumiwa  huyu alikutwa  amehifadhi magunia hayo  porini na akiwa tayari amejiandaa kuyasafirisha.Mtu huyo amekiri kuwa ni mkulima na muuzaji wa Bhangi na alikuwa yuko katika maandalizi ya kuisafirisha Bhangi hiyro.

Jeshi la Polisi bado linaendelea kuwahoji watuhumiwa ili kuweza kuwapata washiriki wengine wanaojihusisha na shughuli hizo na baadaye watawafikisha mahakamani.


No comments

Powered by Blogger.