Polisi wahamishia mashambulizi barabarani
Polisi
imesema watafanya
msako maalumu wa
madereva wasiofuata na kutii sheria za barabarani.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Thobias Sedeyoka
alisema baadhi ya madereva hawafuati sheria na hivyo kusababisha
ajali.
Sedoyeka alisema operesheni hiyo haitafanywa na askari wa usalama
barabarani pekee, bali itashirikisha na wengine.
Alisema watakaokamatwa magari yao yatashikiliwa na wahusika
watalazimishwa kwenda kusoma upya sheria za usalama barabarani,
watakapohitimu watarudishiwa vyombo hivyo.
“Madereva wa aina hii wamekuwa wakisababisha ajali, hivyo lazima
tuandae mkakati maalumu wa kuwadhibiti ili kunusuru maisha ya
wengine,’’ alisema.
No comments