Full-Width Version (true/false)


Polisi yakanusha mwanamke kujifungua nje ya kituo
Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro limekanusha taarifa zinazozagaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii kuhusu kujifungua nje ya kituo cha polisi,  mtuhumiwa (Amina Mbunda) mkazi wa Kisanywa  tarafa ya Mang’ula mkoani humo na badala yake alijifungua wakati akiwa njiani kuelekea hospitali. 
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro  Kamishina Msaidizi wa Polisi Mugabo  Wekwe amesema taarifa zinazosambaa sizo za kweli na kwamba, mtuhumiwa aliwekwa rumande kutokana na kukosekana kwa mtu wa kumuwekea dhamana lakini hata hivyo wakati tukio hilo linatokea hakukua na usafiri karibu.

Kwa mujibu wa Kamanda Wekwe, mama huyo alifikishwa Polisi kituo cha Mang'ula Juni 31 mwaka huu  majira ya saa 12 jioni  na alipofika majira ya saa 9, alianza kulalamika kuwa anajisikia vibaya na anadhani huenda ikawa ni uchungu lakini hakukuwa na gari ya kumfikisha zahanati kwa wakati huo.

Aidha Kamanda Wekwe amefafanua kuwa hata baada ya kutokuwepo na usafiri askari aliyekuwepo zamu alifanya jitihada za kutafuta usafiri wa pikipiki ambapo alimpakia mtuhumiwa pamoja na mama wa jirani na walipofika njiani ndipo mama huyo alipojifungua.

Pamoja na hayo Kaimu Kamanda Wekwe amesema uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea kwa lengo la kubaini kama kuna uzembe wowote uliofanyika.

No comments

Powered by Blogger.