Full-Width Version (true/false)


Rais Magufuli ateua Majaji wawili

Leo June 3, 2018 kuna hii ya kuifahamu toka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  amemteua Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi kuwa Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Kabla ya uteuzi huu Jaji Dkt. Feleshi alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Iringa.

Jaji Dkt. Feleshi anachukua nafasi ya  Jaji Ferdinand Leons Katipwa Wambali ambaye ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.

Jaji Dkt. Feleshi pamoja na Majaji wawili Ferdinand Leons Katipwa Wambali na Mwanaisha Athuman Kwariko walioteuliwa kuwa Majaji wa Mahakama ya Rufani wataapishwa Juni 4, 2018 saa 9:00 Alasiri, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

No comments

Powered by Blogger.