Full-Width Version (true/false)


RAIS Magufuli kuzindua programu ya kuendeleza kilimo kesho

RAIS John Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa programu ya kuendeleza sekta ya kilimo awamu yUzinduzi huo utafanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam na Rais Magufuli ataambatana na wageni wengine wa kitaifa na kimataifa akiwamo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan. 

Wengine ni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, mawaziri wa sekta za kilimo pamoja na wadau wote wa sekta hiyo. 

Taarifa ya uzinduzi wa programu hiyo ya kuendeleza sekta ya kilimo nchini ilitolewa jana na Waziri wa Kilimo, Dk. Charles Tizeba, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. 

Dk. Tizeba alisema, wizara za kisekta zikijumuisha Wizara ya Kilimo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Wizara ya Viwanda, Biashara naa pili (ASDP II)  kesho. 

Uwekezaji, Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Wizara ya Maji na Umwagiliaji ndizo zenye jukumu la kuhakikisha ASDP II inakuwa na mafanikio makubwa nchini na kuwa mkombozi wa wananchi katika kilimo. 

Alisema kuwa ASDP II itatekelezwa katika mikoa na wilaya zote kwa kuzingatia mazao ya kipaumbele kufuatana na ikolojia ya kilimo ya kanda kwa miaka kumi (10) kwa vipindi viwili vya miaka mitano mitano na kipindi cha kwanza kitaanza 2018/19 hadi 2023/24. 


Katika hatua nyingine Dk. Tizeba alitaja lengo la programu hiyo kuwa ni kuleta mageuzi katika sekta ya kilimo ili kuongeza uzalishaji na tija katika kilimo, mifugo na uvuvi; kuongeza pato la wakulima, wafugaji na wavuvi, kuongeza pato la taifa na kuwa na uhakika wa usalama wa chakula na lishe. 

Aidha, programu hiyo itatekeleza sera mbalimbali kama vile Sera ya Kilimo ya Taifa, Sera ya Mifugo ya Taifa, Sera ya Uvuvi, Sera ya Masoko ya Mazao ya Kilimo, Sera ya Umwagiliaji ya Taifa, Sera ya Usalama wa Chakula na Lishe, Sera ya Ugatuaji Madaraka, Sera ya Maendeleo ya Ushirika na Sera ya Mashirikiano kati ya Sekta za Umma na Sekta Binafsi.

No comments

Powered by Blogger.