Full-Width Version (true/false)


Rais Trump atofautiana na nchi washirika


 Mazungumzo katika mkutano wa mataifa yalioendelea kiviwanda duniani G7 yanayofanyika nchini Canada yameshindwa kutatua tofauti zilizopo kati ya rais wa Marekani Donald Trump na viongozi wa mataifa mengine wanachama. 

Washirika wa Marekani wamekasirishwa na hatua ya rais Trump ya hivi karibuni kutoza ushuru vyuma na bidhaa za aluminium , hatua inayozua hofu ya kuzuka kwa vita vya kibishara.

Haijulikani iwapo makubaliano ya pamoja yatawekwa hadharani baada ya kukamilika kwa mkutano huo ambapo tofauti hizo zilionekana hadharani kabla ya kuanza kwa mkutano leo.

Tofauti kati ya Trump na viongozi wengine sita ni zaidi ya tofauti za kibishara zilizopo- zinashirikisha hali ya tabia nchi, uhusiano na Iran na mgogoro kati ya Israel na Palestina.

No comments

Powered by Blogger.