Full-Width Version (true/false)


Rais wa Kenya atangaza vita
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema kuwa maofisa kadhaa waandamizi wa serikali watakamatwa na kushtakiwa katika mapambano yanayoendelea dhidi ya ufisadi. 

Akiwahutubia wananchi katika maadhimisho ya Siku ya Madaraka yaliyofanyika leo katika Uwanja wa Kinoru, Rais Kenyatta amesema mpaka sasa amefurahishwa na idadi ya waliokamatwa na akaongeza kuwa uongozi wake hautakuwa na msamaha na watu hao.

“Nawataka maofisa, hasa waandamizi ambao wametuhumiwa moja kwa moja katika kashfa ya ufisadi wajue hawana nafasi katika serikali yangu na ni kwa wao kwenda jela basi hatimaye lazima ushughulikiwe kwa nguvu zote"amesema Kenyatta.

Ripoti kadhaa kuhusu kashfa ya ufisadi wa mabilioni ya shilingi na ambayo inaweza kuathiri mafanikio ya chama cha Jubilee sasa zinamwangazia Rais Kenyatta mwenyewe.

No comments

Powered by Blogger.