Full-Width Version (true/false)


Rais wa shirikisho la soka Zanzibar (ZFA) ajiuzuluRais wa Chama cha Soka Visiwani Zanzibar (ZFA), Ravia Idarous Faina ameandika barua rasmi ya kujiuzulu nafasi yake na sasa wataungana na makamu wa urais ZFA Unguja, Mzee Zam Ali na Mkurugenzi wa Ufundi, Abdulghan Msoma ambao walitangaza kujiuzulu mwishoni mwa mwezi Mei, mwaka huu. 

Katibu Mkuu wa ZFA, Mohammed Ali Hilali (Tedy) amethibitisha kupokea barua hiyo ya Ravia. 

“Ni kweli ameandika barua ya kujiuzulu nafasi yake, barua ameileta leo Jumatano saa 9 za mchana.” alisema Tedy. Ravia alipokea kijiti hicho cha urais kutoka kwa Amani Ibrahim Makungu tangu mwaka 2013.

No comments

Powered by Blogger.