Full-Width Version (true/false)


Ramadhan: 'wanawake waanaavyopata tabu kula wakiwa kwenye hedhi

 
Wanawake wa kiislamu katika mitandao ya kijamii wamekuwa wakizungumzia changamoto wanazokumbana nazo wakati wanapokula wakati wanapokuwa katika hedhi wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Baadhi yao wanasema kuwa hujificha kutoka kwa ndugu zao wa kiume ili kutoonekana ama hata kudanganya kwamba wako katika hedhi.

Sophia Jamil aliambia BBC : Watu wengine hawataki kukiri tatizo hili hutokea kwa sababu huliona kama kwenda kinyume na dini ya kiislamu lakini kuna tatizo.

Wakati wa Ramadhan , Waislamu hufunga wakati jua linapotoka na kufungua jua linapotoka saa za jioni bila kula chakula ama kunywa maji. 

Hatahivyo wakati mwanamke anapokuwa katika hedhi hawezi kufunga. Lakini licha ya hilo, wanawake wengine hawawezi kuzungumza na ndugu zao wa kiume kuhusu hedhi
"Mamaangu alikuwa akiniambia , kwamba unapokuwa katika hedhi usiwaambie wanaume, ni wanawake pekee ndio wanaojua, alisema mwanablogu huyo wa urembo mwenye umri wa miaka 21.

"Hivyobasi kila nilipokuwa nikinywa maji na kumuona babaangu akija nililazimika kuweka chini kikombe cha maji na kuondoka. Mamangu alikuwa akiniletea chakula chumbani kisiri na kuniambia nile kwa utulivu."

Sophia ambaye anaishi mjini New York na wazazi wake wanatoka Pakistan anasema: Wakati ndugu yangu aliponishika nilikuwa na chakula mdomoni na akaniangalia vibaya. 

''Ndugu zangu hupenda kutaka kunishika nikila ili kuniabisha. Natamani ningekuwa na ujasiri wa kusema kwamba ni jambo la kawaida na kwamba dini yangu inaniruhusu kutofunga kwa sababu sina usafi wa haja''.

Sophia anasema kuwa hedhi ni mada ya aibu ambayo mamake hakumuelezea kwamba atakumbana nayo atakapofikisha umri wa kubalehe. 

''Nadhani hedhi inafaa kuwa kitu ambacho wanawake wanamiliki , hii tabia inafaa kukomeshwa . Kunafaa kuwa na mijadala zaidi na kwamba ni jukumu la vizazi vya sasa kuleta mabadilko hayo'', anasema. 

Sheria ya Ramadhan
Wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhan mtu hafai kula kunywa wala kushiriki katika tendo la ngono kutoka alfajiri hadi jioni. 

Lengo la kutaka kufunga ni sharti lifanyike kabla ya alfajiri. Nia hiyo inaweza kufanywa wakati wa chakula cha Suhoor ama daku.

Wanawake walio katika hedhi hawawezi kufunga, kusoma kitabu kitakatifu cha Quran ama kuingia msikitini. Pia sio lazima kwa mjamzito kufunga wakati wa mwezi wa Ramadhan ,wakati unapokuwa mgonjwa , unapokuwa na umri mkubwa kama vile wazee, unapokuwa na tatizo la kiakili, unapokabiliwa na njaa ama kiu kikali, unaposafiri ama hata iwapo maisha yako yatakuwa hatarini iwapo hautafungua.
Rais wa muungano wa wanafunzi wa Kiislamu , Sabreen Imtair, aliambia BBC alitaka kuwasaidia watu kuzungumzia kuhusu changamoto wanazopitia wakati wa hedhi na akachapisha ujumbe katika mtandao wa Twitter ili watu kuzungumzia mitandaoni.
Alisema: "Familia yangu iko wazi kuhusu maswala kama haya lakini baadhi ya wasichana hususana wakati wa Ramadhan hawawezi kula mbele ya ndugu zao wa kiume na uhisi kuwa wachafu na wenye aibu wakati wa hedhi.."
"Kuna unyanyapaa mkubwa ," anasema msichana huyo mwenye umi wa miaka 18. "kuficha hedhi yako na kuhisi aibu kunawafanya watu kuona swala hilo ni la aibu zaidi. Linabadilisha vile watu wanavyofikiria kuhusu wanawake''

Uzoefu wa Sabrina upo tofauti. Anaweza kula na kunywa wakati wa Ramadhan mbele ya familia yake. 

''Nilienda kununua chakula .Ndugu yangu alikuwa amefunga na akaniuliza kwa nini ninanunua chakula. Nilipomwambia kwamba niko katika hedhi aliniambia ni sawa na akakubali''.
Hatahivyo, Sabreen anatambua umuhimu wa kuzungumza wazi kuhusu hedhi : Mamangu amenifunza njia za kutumia sodo na kukabiliana na damu lakini sio kuwaambia watu kuhusu changamoto hiyo, anasema.

''Sikuweza kuzungumza kuhusu swala hilo na watu hadi hivi karibuni. Ni swala nyeti sana lakini sote tuna hedhi, ni sawa tulifanye liwe swala la kawaida''.

No comments

Powered by Blogger.