Full-Width Version (true/false)


Roma amnyoshea kidole Prof. JayRapa Roma Mkatoliki ambaye mpaka sasa anatamba na wimbo wake 'Zimbabwe' amefunguka na kudai Mbunge wa Mikumi (CHADEMA) ambaye pia ni msanii hip hop Bongo, Profesa Jay anasifa zote za kuitwa mkongwe wa bongofleva licha ya kuwa ndio role model wake. 


Roma ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha FRIDAY NIGHT LIVE 'FNL' inayorushwa kutoka EATV kila Ijumaa baada ya kuulizwa swali na muongozaji wa kipindi hicho kama Joseph Haule maarufu kama Prof. Jay anaweza akawa na sifa ya kuitwa msanii mkongwe wa hip hop.

"Prof. Jay anafaa kuitwa mkongwe kwenye huu muziki kwasababu ni miongoni mwa wasanii walioweza kupigania huu muziki vile vile ni kwangu mimi ndio 'role model' wangu", amesema Roma.

Aidha, Roma amesema sio kweli kwamba wasanii wa zamani wanakataa kuitwa wakongwe kama baadhi ya watu wanavyofikilia.

"Issue sio ukongwe bali kuna baadhi ya makundi hayapewi nafasi kwenye 'media house' mchongo ndio upo hapo hizo nyingine zote ni michongoma kwa hiyo ingekuwa watu wanawaita wakongwe halafu wanapata kile wanachostahili wala wasingeweza kulaumu", amesisitiza Roma.

No comments

Powered by Blogger.