Full-Width Version (true/false)


Ronaldo atimiza ndoto za mtoto wa miaka minne, apewa ujumbe mzito wa kombe la dunia (+video)

 
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ureno na klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo Jumamosi iliyopita akiwa na wachezaji wa timu yake ya taifa waliondoka nchini Ureno kuelekea Urusi kwa ajili ya michuano ya kombe la dunia, safari ambayo imetimiza ndoto za mtoto Rafaela Agostinho.

Ronaldo wakati akiingia kwenye Uwanja wa ndege wa Lisbon Portela aliitwa na mtoto aliyetambulika kwa jina la Rafaela Agostinho akimtaka amsainie autograph yake.

Mtoto huyo ambaye aliruka kwenye kizuizi na kumkimbilia Ronaldo, mama yake mzazi na mtoto huyo amedai kuwa Rafaela alikuwa anamsumbua kwa miaka miwili mfululizo ikiwemo kumuomba jezi za Ronaldo.

“Mtoto wangu naona ametimiza ndoto yake ya kukutana na Ronaldo kwani kwa miaka miwili nimekuwa nikimuahidi kwamba atakutana naye, Rafaela anaipenda sana timu ya taifa (Ureno) na alisema anataka kumwambia kitu Ronaldo, nadhani unamuona analia kwa furaha,”amesema Mama yake na Rafaela.

Mama Rafaela amesema amesafiri kutoka Braga hadi Lisbon ili kutimiza ahadi kwa mtoto wake ambaye amekuwa akimsumbua tangu mwaka 2016.

Akielezea ujumbe aliomwambia Ronaldo, Rafaela amesema amemwambia kuwa asisahau kurudi na Kombe la Dunia kwani amekuwa akiliona kwenye Tv tu hajawahi kulishika.

Timu za taifa za Ureno, Argentina na Misri ni moja ya timu zilizowasili nchini Urusi wikiendi iliyopita kwa ajili ya michuano ya kombe la dunia.Tazama video ya tukio hilo hapa chini

No comments

Powered by Blogger.