Full-Width Version (true/false)


Sababu inayomfanya Kijana huyu kuonekana kama Mzee

Kijana Xiao Cui raia wa China ana miaka 18 lakini muonekane wake ni kama mtu wa miaka 80.

Xiao ambaye bado ni Mwanafunzi wa sekondari anasumbuliwa na tatizo la kiafya linalosababisha misuli na ngozi yake ya uso kusinyaa na kumfanya aonekane mzee sana.

Madaktari bado wanahangaika kutatua tatizo hilo la kiafya la kijana huyo ambaye anafanya vizuri sana shuleni mpaka amepachikwa jina la ‘Superman’ na Wanafunzi wenzake kwa uwezo wake kufanya vizuri katika nyanja tofauti tofauti.

Kwa upande mwingine waalimu katika shule yake wanamsifia sana kijana huyo kuwa ijapokuwa anakabiliwa na changamoto hiyo lakini bado anafanya vizuri sana na wanasema kuwa Xiao ataenda kusoma katika chuo kikuu cha China na kufanikiwa kwa kila jambo analolitaka.

Aidha kijana huyo anasema kuwa kuna nyakati watu humtania kutokana na tatizo lake  na wakati mwingine hukasirika lakini baadae huwapuuzia.

No comments

Powered by Blogger.