Full-Width Version (true/false)


Salah amnyima Ramos usingizi

 
Mambo bado magumu unaambiwa, na sasa beki wa kati wa Real Madrid, Sergio Ramos amedaiwa kubadili namba ya simu yake ya mkononi baada ya ile ya kwanza kupokea meseji nyingi za vitisho vya kuuawa, baada ya lile tukio lake na Mohamed Salah kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Jumamosi iliyopita. 

Ramos aliwaacha mashabiki wa Liverpool na Misri wakiwa na hasira kubwa baada ya kudaiwa kumuumiza Mo Salah na kushinda kumaliza mechi hiyo ya fainali iliyomalizika kwa Real Madrid kuibuka na ushindi wa mabao 3-1. 

Salah aliumia bega na ripoti zinadai kwamba atakuwa nje ya uwanja kati ya wiki mbili hadi tatu, hivyo amefufua matumaini ya kuwapo kwenye fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika Russia baadaye mwezi huu.

No comments

Powered by Blogger.