Full-Width Version (true/false)


Sam wa Ukweli kuzikwa kesho Bagamoyo

 
Mwanamuziki Sam wa Ukweli amefariki dunia Juni 6, 2018, atazikwa kesho saa tisa nyumbani kwao kiwangwa Bagamoyo. 

Akizungumza na MCL Digital meneja wa Sam ,Amri Aliamini amesema mwili wa Sam utasafirishwa kesho saa mbili asubuhi watatokea Mochwari kwenda Bagamoyo, lakini leo watafanya kikao saa sita mchana kwa Mjomba wake anayeitwa Said Yanga anayeishi Tandale. 

Sam alizidiwa jana saa mbili usiku akiwa studio ya Asound akirekodi, akakimbizwa Hopitali ya Palestina saa nne usiku na kufariki akiwa njia, lakini kabla ya hapo alikuwa anasumbuliwa mara kwa mara na Maralia na homa ya manjano kwa mwezi mmoja na nusu akiwa Singida kwenye shoo. 

"Mimi nachojua chanzo cha kufariki Sam ni kuumwa Maralia na Homa ya Manjano, baada ya kuzidiwa akiwa studio ya Asound iliyopo Mabibo saa mbili usiku, tulipofika Hospitali ya Palestina akahifadhiwa kwa muda na baadae tukaambiwa tumpeleke Mwananyamala maana pale hawahifadhi," alisema Amri.

No comments

Powered by Blogger.