Full-Width Version (true/false)


Samatta, Wanyama wahudhuria ufunguzi wa Ndondo Cup

 


Mastaa wa soka Afrika Mashariki, Mbwana Samatta na Victor Wanyama wamewateka mashabiki wa soka waliofika kushuhudia ufunguzi wa mashindano ya Ndondo Cup. 

Samatta anayekipiga Genk ya Ubelgiji na Mkenya Wanyama anayecheza Totternham Spurs ya England ni miongoni wageni walioshudia mechi kati Mabibo FC dhidi ya Keko Furniture kwenye Uwanja wa Kinesi. 

Wanyama alikuwa wa kwanza kufika na alikuwa miongoni mwa waliokagua timu, lakini Samatta alichelewa na kukuta ukaguzi ukiwa umeshafanyika jambo lililoamsha shangwe kwa mashabiki waliojitokeza uwanjani hapo. 

Mashindano ya Ndondo Cup yamezinduliwa rasmi leo na Mkurugenzi wa Michezo, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,Yusuph Singo.

No comments

Powered by Blogger.