Full-Width Version (true/false)


Sekta ya kilimo yachangia asilimia 65.5 ya ajira nchini

Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa sekta ya kilimo inachangia asilimia 65.5 ya ajira zote nchini.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo, Juni 4, 2018 wakati wa  programme ya kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya Pili katika Ukumbi wa Mwl Nyerere jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa asilimia 30 sekta ya kilimo inachangia pato la Taifa.

“Serikali za awamu mbalimbali za nchi yetu, hivi punde Waziri wa Kilimo amesema Sekta ya kilimo ina changia asilimia 100 ya chakula hapa nchini na inachangia asilimia 30 ya pato la taifa asilimia 65.5 ya ajira zote nchini na asilimia 65 ya marighafi zote za viwanda na takribani asilimia 30 za mauzo ya nje ambayo kila Mtanzania anabudi kujivunia ,” amesema Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli aliwakumbusha Mabalozi wa Tanzania walioko nje kuwa moja ya majukumu yao ni kutafuta masoko kwa ajili ya bidhaa zetu za kilimo.

No comments

Powered by Blogger.