Full-Width Version (true/false)


Serikali imewataka walimu wawe na subira

“Walimu wawe na subira”- Serikali


Serikali imewataka walimu wa Sekondari waliohamishiwa kufundisha shule za msingi, kuendelea kuwa na subira wakati Serikali ikijipanga kutenga fedha za kuwalipa walimu hao kutokana na uhamisho uliofanyika. 

Hayo yamesemwa leo Juni 5, 2018 Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Joseph Kakunda, katika kipindi cha maswali na majibu na kuongeza kuwa katika mwaka mpya wa fedha 2018/2019 Serikali itahakikisha walimu wote wenye sifa stahiki watalipwa fedha hizo.

“Wengine tayari walikuwa wameshapewa na Halmashauri pesa za kujikimu, sisi tunaomba walimu wote wenye stahiki za kulipwa stahili, basi waweze kuwa na subira unapoanza mwaka ujao wa fedha kwa bajeti mpya tutahakikisha wamelipwa stahili zao” amesema Kakunda.

Kakunda ameongeza kuwa, kwa mujibu wa agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alilotoa February mwaka huu la kukataza watumishi wa Serikali kuhamishwa mpaka kuwepo na fedha za kuwalipa, hivyo zoezi la ulipaji litahusisha walimu ambao walikuwa wamehamishwa kabla ya agizo hilo.

Naibu Waziri Kakunda, alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Karagwe, Innocent Bashungwa, aliyetaka kujua ni lini Serikali itawalipa walimu 131 katika Jimbo lake ambapo wanaidai Serikali kiasi cha shilingi milioni 430 baada ya uhamisho huo.

Julai 4, 2017 Serikali ilitangaza kuhamisha walimu wa Sekondari wanaofundisha masomo ya sanaa kupelekwa kufundisha shule za msingi ili kuziba pengo la uhitaji wa walimu taktribani 47,151 katika shule za msingi.

No comments

Powered by Blogger.