Full-Width Version (true/false)


Serikali isipopeleka bungeni muswada kuhamia Dom, hakuna Bunge Oktoba

 

Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema kama Serikali haitapeleka Bungeni muswada wa Serikali kuhamia Dodoma, hakutakuwa na mkutano wa Bunge Oktoba. 

Spika Ndugai ametoa kauli hiyo leo bungeni Juni 4, 2018 akimjibu Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa aliyesema mpango wa kuhamia Dodoma haupo katika mpango wa Taifa. 

Amesema tatizo lililokuwepo huko nyuma ni kutotekelezwa kwa azimio hilo la Dodoma kuwa makao makuu ya nchi. 

"Kama muswada wa kuhamia Dodoma hautasomwa kwa mara ya kwanza katika mkutano huu wa Bunge, Bunge la Oktoba halitakuwepo," amesema Spika Ndugai. 

"Waziri (Jenista) Mhagama, mwambie AG (Mwanasheri Mkuu wa Serikali) kabisa, kama muswada huu hautakuja, hakuna muswada wowote wa Serikali utakaoingia katika Bunge hili," ameongeza.

No comments

Powered by Blogger.