Full-Width Version (true/false)


Serikali yaipa angalizo TRA
Serikali imeiagiza Mamlaka ya Mapato Nchini TRA kuhakikisha wanawatembelea wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kama wamachinga katika maeneo yao kwa lengo la kuwaelimisha na  waweze kuchangia pato la serikali kupitia biashara wanazofanya.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashantu Kijaji wakati akifunga mkutano wa siku tatu wa shirikisho la umoja wa wamachinga shiuma Jijini Dodoma.

Dkt. Kijaji amesema mamlaka hiyo kupitia wafanyabiashara na kuwatambua kutasaidia kwenda katika taasisi za kifedha kukopa pamoja na kutambuliwa wakati wa usajili wa vitambulisho vya taifa zoezi linaloendeshwa na  idara ya uhamiaji na nida.

Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Simon Siro aliyewakilishwa na Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema watu wanaojipatia mali za wamachinga kwa kuwanyanganya na kwenda kuzitumia kinyume cha utaratibu watachukuliwa hatua.

No comments

Powered by Blogger.