Full-Width Version (true/false)


Serikali yapiga marufuku kujadili Trilioni 1.5
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mh. Jenista Mhagama amewataka Wabunge kutojadili suala la Trilion 1.5 ndani ya bunge kutoka kwenye ripoti ya CAG, hadi kamati ya PAC itapowasilisha ripoti yake. 

Waziri Mhagama ametoa kauli hiyo leo Bungeni baada ya Mbunge wa Kibamba John Mnyika kusimama na kuihoji Serikali kuhusu fedha hizo, ambazo ziliacha gumzo kubwa kwa umma na wanasiasa baada ya ripoti ya CAG kutolewa mapema mwa mwezi April mwaka huu.

Suala la upotevu wa Trilioni 1.5 kwenye ripoti ya CAG imeibua mjadala mkubwa kwa watu mbali mbali, huku wakiituhumu serikali kwa upotevu wake, licha ya Wizara ya Fedha kutoa mchanganuo wa taarifa hiyo na kuonesha kwamba hakuna pupotevu wa fedha wa trilioni 1.5.

No comments

Powered by Blogger.