Full-Width Version (true/false)


Simba imerejea nchini Usiku wa manane,Kocha Agoma KuzungumzaKikosi cha Simba kimerejea nchini usiku wa saa saba  kikitoea, Nakuru, Kenya ambako kilienda kushiriki mashindano ya SportPesa Super CUP.

Kikosi hicho kimerudi ikiwa ni baada ya kupoteza mchezo wa fainali kw ajumla ya mabao 2-0 dhidi ya Gor Mahia uliopigwa jana kwenye Uwanja wa Afraha.


Kwa mujibu wa Ofisa wa Habari wa Simba, Haji Manara, amesema wamewahi kurejea kwa ajili ya halfa maalum ya ugawaji wa tuzo za wachezaji wao unaofanyika leo kwenye Hotel ya Hyatt Regency Hotel jijini Dar es Salaam.


Kocha Masoud Djuma alipofuatwa na mwandishi  ili aweze kuzungumzia mchezo wa fainali pamoja na michuano hiyo kwa ujumla alisema amechoka sana na anahitaji kupumzika huku akitoa ahadi ya kumpigia simu mwandishi huyo kesho.


“Nimechoka sana, naomba uniache nikapumzike kwanza tafadhali, kesho mimi ndiye nitakutafuta tuzungumze. Sijawahi kukataa kuzungumza nanyi lakini leo mtanisamehe,” alisema Masoud.
Simba imeshika nafasi ya pili baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-0 toka kwa Gor Mahia jioni ya jana na kuwaacha wenyeji hao wakijitwalia tiketi ya kwenda kucheza na Everton kwenye uwanja wa Godson Park nchini Uingereza.

tazama video hii hapa chini wakiwasili uwanja wa ndege.

No comments

Powered by Blogger.