Full-Width Version (true/false)


Simba, Yanga wagoma kulala hoteli moja Kenya

 

Miamba ya soka Tanzania, Simba na Yanga wamehamishia bifu lao nchini Kenya baada ya kugoma kulala kwenye hoteli moja jijini Nakuru. 

Taarifa zaidi zimeekeza kuwa viongozi wa klabu hizo mbili walikataa kabisa wachezaji wao kuchukuiliwa vyumba kwenye Hoteli ya Midlands. Hivyo imewalazimu waandaaji kutafuta hoteli nyingine. 

Kutokana na hali hiyo Yanga watabakia pale Midlands huku Simba wakihamishiwa hadi kwenye Hoteli ya Water Buck. 

“Ni kitu ambacho kimekuwepo kwamba hatuwezi kula kwenye sahani moja au kukutana uso kwa uso hasa asubuhi kabla ya mechi. Hali hiyo hutia mkosi” alinukuliwa kiongozi mmoja wa Simba aliyesafiri na timu. 

Hali hiyo pia imeripotiwa kuwaathiri mashabiki wa timu hizo mbili waliosafiri nao, ambao pia wameamua hawatajichanganya hivyo kila kundi ikiamua kusaka hoteli za malazi mbali na wenzao. 

Yanga ni mabingwa mara 27 wa Ligi Kuu ya Tanzania huku Simba wakitwaa ubingwa huo mara 19. Uhasama wao umedumu kwa miaka mingi tangu timu hizo zilipoasisiwa.

No comments

Powered by Blogger.