Simba, Yanga wakinukisha Kenya

Simba na Yanga
zimeanza mazoezi
ya nguvu nchini
Kenya katika
maandalizi yao ya
kujiandaa na mashindano ya SportPesa Super Cup yanayotarajiwa
kuanza Jumapili mjini Nakuru.
Katika mazoezi hayo Simba ilimtambulisha mshambuliaji mpya
Marcel Kaheza waliyesajili kutoka Majimaji, wakati Yanga
mkongwe Amiss Tambwe amerejea kikosini tayari kwa
mashindano hayo.
Ratiba ya mashindano hayo inaonyesha Yanga itakata utepe Juni 3
dhidi ya KK Home Boys e kwenye Uwanja wa Afraha, mjini
Nakuru endapo itashinda mchezo huo wa mtoano, itasubiri
mshindi wa mechi kati ya Simba na K Sharks utakaopigwa Juni 4.
Kama Simba na Yanga zote zitashinda mechi zao za kwanza
zitakutana katika mchezo wa nusu fainali utakaopigwa Juni 7
nchini humo.
Timu zingine za Tanzania zinazochuana ni JKU ya Zanzibar
ambayo itacheza mechi yake ya kwanza na bingwa mtetezi, Gor
Mahia hapo Juni 4, wakati Singida United yenyewe itavaana na
AFC Leopards.
Mtanange wa fainali utapigwa Jumapili ya Juni 10, kuanzia saa
tisa alasiri.
Kabla ya mechi hiyo, kutakuwa na mchezo wa kusaka
mshindi wa tatu utakaorindima kuanzia saa sita mchana.
Bingwa wa mashindano hayo atajinyakulia kitita cha dola 30,000
pamoja na kupata tiketi ya kwenda kucheza mechi ya kirafiki ya
kimataifa dhidi ya Everton nchini England.
No comments