Full-Width Version (true/false)


Singida United mshindi wa tatu SportPesa Super Cup

 
Klabu ya Singida United kutoka Tanzania imefanikiwa kuwa mshindi wa tatu katika Michuano ya SportPesa Super Cup baada ya kuifunga Kakamega HomeBoys kwa penati.

Singida imeishinda Kakamega kwa penati 4-1,  baada ya dakika 90 za mchezo kumalizika wakiwa wamefungana goli 1-1.

Kakamega ndio ilikuwa ya kwanza kupata goli kupitia kwa Wickleaf Opondo mnamo dakika ya 4. Lakini Singida waliweza kusawazisha kupitia kwa Danny Lyanga dakika ya 61


Katika mchezo huo Nahodha wa Singida Deus Kaseke ametangazwa kuwa mchezaji bora wa mechi ya mshindi wa tatu akichaguliwa na jopo la makocha kutoka Everton.

No comments

Powered by Blogger.