Full-Width Version (true/false)


Singida United yaingia nusu fainali SportPesa Super Cup

Singida United imeungana na Simba kuingia hatua ya nusu fainali ya mashindano ya SportPesa Super Cup kwa ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya AFC Leopards wa njia ya matuta.


Ushindi huo umepatikana na kuiwezesha Singida United kutinga hatua hiyo baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya 0-0.


Kipa wa Singida, United, Manyika Junior, ameibuka shujaa wa mchezo huo baada ya kuokoa penati mnamo kipindi cha pili kabla ya dakika 90 hazijamalizika.


Matokeo yanaifanya Singida iungane na Simba huku Yanga na JKU kutoka Tanzania zikiwa tayari zimeshaaga mashindano.

No comments

Powered by Blogger.