Singida united yamnasa nyota kutoka Prisons, asaini miaka mitatu
Klabu
ya Singida United imeingia mkataba wa miaka mitatu na kiungo, Kazungu
Mashauri, aliyekuwa akiichezea Tanzania Prisons ya Mbeya.
Usajili huo umekuja ikiwa ni siku kadhaa zimepita klabu hiyo itoke kumtangaza aliyekuwa mshambuliaji wa Mbao FC, Habibu Kyombo.
Kazungu
amejiunga na Singida ambayo ipo mjini Nakuru iijiandaa na mchezo wa
michuano ya SportPesa Super Cup dhidi ya AFC Leopards.
Singida
itakuwa na kibarua hicho ikiwa pamoja na Simba kama timu pekee
zilizosalia kwenye mashindano hayo baada yaYanga na JKU ya Zanzibar
kutolewa.
No comments