Siri imefichuka, Zimbwe alikataa kupiga penalti, kocha mfaransa akasisitiza
Beki
Mohamed Zimbwe maarufu kama Tshabalala alikataa kupiga mkwaju wa
penalti kabla ya kulazimishwa kufanya hivyo na kocha wake, Pierre
Lechantre.
Zimbwe
alikosa penalti wakati Simba ikiivuka hadi nusu fainali ya Kombe la
SportSuper Cup. Hiyo ilikuwa ni mara yake ya tatu akikosa.
Moja
ya vyanzi vilieleza kwamba Zimbwe maarufu alimuomba kocha wake asipige,
lakini kwa kuwa siku hiyo alikuwa nahodha alimlazimisha apige.
"Kocha alilazimisha alitaka akapige, alipomuomba asipiga alimuambia lazima aheshimu uwezo wake," kilieleza chanzo.
Taarifa
nyingine zilileza kwamba Pamoja na Tshabalala, Paul Bukaba yake aliomba
asipige penalti lakini kocha huyo raia wa Ufaransa alisisitiza lazima
apige, naye alikosa.
Kikosi cha Simba kimeapa kubadilika katika mechi yake ijayo ya michuano ya Kombe la SportPesa Super Cup.
Kocha Msaidizi wa Simba, Masoud Djuma amesema wanaamini hawakucheza katika mechi yao iliyopita ya michuano hiyo mjini Nakuru.
No comments