Full-Width Version (true/false)


Siri ya mapacha wliofariki kupewa majina ya Maria na Consolata
Mkuu wa Shirika la Maria Consolata, Jane Nugi amesema watu wengi wamekuwa na maswali kuhusu majina ya Maria na Consolata yanayofanana na shirika lililowalea akieleza kuwa baada ya kuzaliwa mapacha hao, wazazi wao waliamua kuwakabidhi kwao kulingana na hali waliyokuwa nayo na hivyo kutakiwa kuwapatia majina. 

“Baba yao mzazi Mwakikuti aliposhauriwa kuwabatiza baada ya kuzaliwa kutokana na hali waliyokuwa nayo aliomba masista watoe majina hivyo yule aliyekuwepo akawaita Maria na Consolata,” amesema. 

Sista Jane amesema waliwalea watoto hao katika mazingira ya kiimani wamjue Mungu na kuwafundisha upendo. Amesema walipomaliza darasa la saba katika Shule ya Msingi ya Ikonda, wilayani Makete waliwapeka Kilolo katika shule yao ya Maria Consolata walikohitimu kidato cha nne. 

Amesema wakiwa huko waliwajengea nyumba na kuwaandalia mazingira mazuri ya kuishi huku wakiwa chini ya uangalizi wa viongozi wa Maria Consolata. Amesema hadi wanamaliza kidato cha sita katika Shule ya Sekondari ya Udzungwa mpaka wanaingia Rucu walikuwa karibu nao kwa kila hatua.

No comments

Powered by Blogger.