Full-Width Version (true/false)


"Siwezi ku-post picha ya marehemu Sam wa Ukweli"- AlikibaMsanii wa Bongo Fleva mwenye 'hit song' ya 'Mvumo wa Radi' Alikiba amefunguka na kudai sababu kubwa ya yeye kutoka ku-post picha marehemu Sam wa Ukweli katika mitandao ya kijamii ni kutokana na imani ya dini yake ya kiislamu kutomruhusu kufanya hivyo na wala sio kitu kingine. 

Alikiba ametoa kauli hiyo leo Juni 07, 2018 wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam baada ya kuwepo lawama nyingi kwa wadau mbalimbali wa muziki wakidai Kiba hana ushirikiano na wenzake hata katika masuala ya msiba huwa a-post picha ya marehemu na mambo mengine. 

"Nataka niliweke sawa hili kwa jamii, mimi dini yangu hainiruhusu ku-post picha ya aina yoyote ya marehemu katika mitandao ya kijamii ndio maana watu hawanioni nikifanya hivyo lakini huwa natuma salamu za rambirambi kwa familia nasio kwa kujionesha machoni mwa watu", amesema Alikiba.

Pamoja na hayo, Alikiba ameendelea kwa kusema "kusema ukweli nimeguswa na kifo cha msanii mwenzetu Sam wa Ukweli. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.

Sam wa Ukweli amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Palestina Sinza alipokuwa amelazwa kwa ajili ya matibabu kutokana na maradhi yaliyokuwa yakimsumbua.

No comments

Powered by Blogger.