Full-Width Version (true/false)


Spika Ndugai ataja cheo chake kingine


 Spika wa  Bunge la Tanzania, Job Ndugai katika hali ya utani leo bungeni  amewataka wabunge wake kutambuana kwa vyeo tofauti na vile vya uwakilishi wa wananchi katika jumba hilo ambapo amesema yeye ni Mzee wa Kanisa lakini hawamtambui. 

Spika amechomeka kauli hiyo  leo mapema katika Kikao cha 48, Mkutano wa 11 kipindi cha maswali na majibu ambacho  mjini Dodoma  wakati Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza alipokuwa akiju swali la la Mbunge Taska Restuta Mbogo kwamba  "Ni lini serikali itawatambua, Machifu na Watemi wa makabila mbalimbali ili waweze kusaidia kurekebisha maadili katika jamii za kitanzania?

Katika majibu yake, Waziri Shonza amesema kuwa serikali inawatambua, machifu wa mila za Tanzania na ndiyo maana hata katika shughuli za kiserikali huwa wanashirikishwa huku akitolea mfano shughuli za mbio za mwenge.

Mh. Shonza amesema kwamba  "Serikali inawatambua na itazidi kuwatambua watemi na machifu kwa kuwa ni njia moja wapo ya kuenzi na kudumisha mila pamoja utamaduni".

Akiongeza majibu ya swali hilo, Waziri wa Wizara hiyo  Dkt. Harisson Mwakyembe amesema kuwa wiki iliyopita alifanikiwa kuhudhuria katika maadhimisho ya kituo cha kumbukumbu ya utamaduni wa Kabila la Wasukuma huko Bujora Mwanza, ambapo  Machifu wa wengi wa Kisukuma walihudhuria ambapo yeye alipata bahati ya kutunukiwa cheo cha 'Manji Mkuu wa ngoma', na kuongeza kuwa "nafasi ya machifu ni suala ambalo linaangaliwa kwa makini ili kuleta mjadala mpana ikiwa pamoja na kutambua nafasi zao kisheria".

Akihitimisha majibu hayo kwa njia ya utani Spika Ndugai amesema "Hasa mliosimama nyie machifu jamani? Tunatakiwa kutambua Tittle za watu, muhimu sana. Mi nawashangaa Mimi Mzee wa Kanisa hamnitambui".

No comments

Powered by Blogger.