Straika ajiapiza Simba
Straika wa Simba,
Marcel Kaheza
'Rivaldo'
amesema,
mpango wake ni
kuona anaitendea
haki jezi namba
10 aliyopewa ndani ya kikosi hicho.
Kaheza tangu ametua ndani ya timu hiyo amekabidhiwa jezi
namba 10 ambayo ilikuwa inavaliwa na Juma Luizio aliyemalizana
na Simba na akaichezea katika michuano ya SportPesa iliyofanyika
nchini Kenya na Wekundu hao kumaliza kwenye nafasi ya pili.
Amesema: "Kama unavyojua jezi hii huwa ni nzito mara nyingi
inavaliwa na watu wazito hivyo nitapambana kadri ya uwezo
wangu kuona naitendea haki kwa kufanya vizuri Simba."
"Binafsi huwa napenda sana kuitumia jezi hii kwa miaka mingi
tangu nianze kucheza ni kipindi kirefu sasa na ilikuwa ikitumiwa
na mchezaji ambaye nampenda zaidi Rivaldo,"amesema Kaheza.
Rivaldo ni mchezaji na nahodha wa zamani wa timu ya Brazil.
No comments