Full-Width Version (true/false)


Takwimu: Tanzania ina ng’ombe zaidi ya milioni 30 .569


 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa kwa Tawimu za sasa zinaonyesha Tanzania ina ng’ombe zaidi ya 30. 569.

Rais Magufuli amesema kuwa Tanzania ni nchi ya pili kwa kuwa na ng’ombe wengi ikiongozwa na Ethiopia ambapo amesema kuwa inawezekana Ethiopia tunawakaribia.

“Tunashika nafasi ya Pili kwa kuwa na idadi kubwa ya Mifugo Barani Afrika ninaambiwa kwa Takwimu za sasa tuna ng’ombe zaid ya milioni 30 .569 sifahamu ndio takwimu zilizokuwa zimetolewa na hivyo tunashika nafasi ya pili baada ya Ethiopia na inawezekana tunawapatapata au kuwakaribia na kuwazidi,” Rais Magufuli ameyasema hayo leo, Juni 4,2018, wakati wa programme ya kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya Pili katika Ukumbi wa Mwl Nyerere jijini Dar es Salaam.

No comments

Powered by Blogger.