Full-Width Version (true/false)


TAMBWE YUKO VIZURI, AANZA KUJIFUA NA YANGA KWA AJILI YA SPORTPESA SUPER


Mshambuliaji Amissi Tambwe wa Yanga amerejea katika hali yake na leo amefanya mazoezi ya pamoja na wenzake.

Tambwe amesafiri na kikosi cha Yanga hadi hapa Nakuru kwa ajili ya michuano ya Kombe la SportPesa Super Cup.


Raia huyo wa Burundi, amekaa nje takribani msimu mzima akiuguza majeraha.


Kikosi cha Yanga kimeanza mazoezi yake ya kwanza kabla ya mechi yao ya kwanza ya michuano ya SportPesa Super Cup, keshokutwa.

Yanga imefanya mazoezi yake ya kwanza mjini Nakuru nchini Kenya, tayari kwa kazi ya keshokutwa dhidi ya Homeboyz.


Yanga iliwasili mjini hapa jana ikitokea jijini Dar es Salaam tayari kushiriki michuano hiyo itakayoshirikisha timu nane, nne zikiwa kutoka Tanzania na nne za hapa Kenya.

No comments

Powered by Blogger.