Full-Width Version (true/false)


Tanzania na Malawi kuendelea kuimarisha uhusiano wa kibiasharaSerikali ya Tanzania inaendelea na jitihada za kuimarisha uhusiano wa kiuchumi na Serikali ya Malawi kupitia sekta ya biashara na uwekezaji ili wananchi waweze kunufaika na fursa mbalimbali zinazopatikana katika nchi zote mbili.


Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla alisema kuwa katika kuimarisha uhusiano huo, Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Malawi zimeandaa Kongamano la Biashara na Uwekezaji litakalofanyika Julai 26 na 27 mwaka huu Jijini Mbeya.

Makalla alieleza kuwa lengo la kongamano hilo ni kuwakutanisha wafanyabiashara na wawekezaji wan chi zote mbili ili kubaini fursa mbalimbali zitakazowezesha kuanzisha na kuendeleza miradi katika sekta za viwanda, usafirishaji, utalii, uvuvi, kilimo, madini, elimu, afya, benki, mawasiliano, Tehama na biashara kwa ujumla.

“Kongamano hili linatarajiwa kuhudhuriwa na washiriki wapatao 500 ikijumuisha wafanyabiashara, wawekezaji, Taasisi za Umma na sekta binafsi kutoka Tanzania na Malawi,” alisema Makala.

No comments

Powered by Blogger.