Full-Width Version (true/false)


Tanzia: Mbunge Majimarefu amefiwa na Mkewe Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephen Ngonyani maarufu 'Profesa Majimarefu’ leo Jumatano Juni 6, 2018 amefiwa na mkewe aliyekuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Akizungumza na MCL Digital leo Mkurugenzi wa mawasiliano wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Aminiel Aligaesha amethibitisha kifo cha mke wa mbunge huyo, kubainisha kuwa aliaga dunia saa 3 asubuhi.

Spika wa Bunge, Job Ndugai akizungumza na MCL Digital, amempa pole Ngonyani pamoja na familia yake.

“Ni kweli amefariki, tumepata taarifa hizo si muda mrefu leo na alikuwa amelazwa kwa muda mrefu katika pale Muhimbili ICU (chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum).

Maofisa wa Bunge wakiwa na Ngonyani wako pale wanaendelea kutoa msaada wa karibu kabla ya kuendelea na taratibu nyingine,” amesema Ndugai.

“Na kwa sababu huyu mama pia alikuwa ni diwani kule Korogwe, Bunge na halmashauri ya Korogwe vijijini tutashirikiana kwa pamoja lakini kwa sasa tunaendelea kuwasiliana na familia ya Majimarefu.”

No comments

Powered by Blogger.