Full-Width Version (true/false)


Tazama Rais Trump na Kim Jong-Un walivyowasili kibabe nchini Singapore kwenye mkutano wao wa kihistoria (+video)

 

Yakiwa yamesalia masaa machache kuanza kwa mkutano wa kihistoria kati ya Rais wa Marekani, Donald Trump na Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-Un tayari wawili hao usiku wa kuamkia leo wamewasili nchini Singapore kama awali walivyowahi kupanga sehemu hiyo kama eneo la kukutania.

Katika msafara wa viongozi wote wawili, Trump hajaonekana kuwa na ulinzi mkubwa ukilinganisha na Kim ambaye gari lake lilizunguukwa na mabodigadi 12.

Mkutano wa Trump na Kim Jong Un ni mkutano wa kihistoria baina ya mataifa hayo makubwa kijeshi na unatarajiwa kufanyika kesho Jumanne Juni 12 katika kisiwa cha Sentosa, nchini Singapore.

Miongoni mwa ajenda kubwa zinazotarajiwa kujadiliwa kwenye mkutano huo hapo kesho ni pamoja na kufikiwa makubaliano rasmi ya kusitisha utengenezaji wa silaha za nyuklia.

Zaidi ya waandishi wa habari 2500 wanatarajiwa kuwepo kwenye mkutano huo wa kihistoria ingawaje muda rasmi wa kuanza kwa mkutano huo hadi sasa haujatangazwa.Tazama walivyowasili viongozi hao wawili

No comments

Powered by Blogger.