Full-Width Version (true/false)


Tetesi za soka Barani Ulaya leo Jumanne June 05,2018

Mshambuliaji wa Liverpool na Senegal Sadio Mane, 26, alikubali kujiunga na Real Madrid kabla ya Zinedine Zidane kujiuzulu kama kocha wa mabingwa hao wa Ulaya. (France Football - in French)
 
Matumaini ya Chelsea ya kumzuia Eden Hazard yamepigwa jeki na hatua ya Zidane kuondoka Real. Raia huyo wa Ufaransa aliambia mabingwa hao wa Uhispania kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 msimu ujao. (London Evening Standard)
 
Zidane alijiuzulu katika Real Madrid kutokana na mipango ya dirisha la uhamisho la msimu ujao. Klabu hiyo ilikuwa ikitaka kumnunua Kipa wa Manchester United na Uhispania David De Gea 27, lakini Zidane hakutaka. Pia alikasirika kwamba mpango wake wa kutaka kumsajili Hazard haikuungwa mkono. (Sun)
 
Leicester imefufua hamu yake ya kumsajili mshambuliaji wa Manchester City na raia wa Uingereza Patrick Roberts, 21, ikiwa ni miongoni mwa dau la £60m ambalo litahakikisha kuwa winga wa Algeria Riyad Mahrez, 27, anajiunga na viongozi hao wa ligi. (Daily Telegraph)
 
Mkufunzi wa Tottenham Mauricio Pochettino alikataa kuwa mkufunzi wa Real Madrid kwasababu hakutaka kuonekana kuwa anapenda fedha zaidi. (Daily Mail)
 
Arsenal inapanga uhamisho wa Marouane Fellaini, 30, ambaye kandarasi yake katika klabu ya Manchester United inakamilika mwezi huu. (Daily Mirror)
 
Beki wa kulia wa Ureno Diogo Dalot, 19, atafanyiwa uaguzi wa matibabu wiki hii kabla ya kujiunga na klabu hiyo kutoka Porto. (Sky Sports)

No comments

Powered by Blogger.