TFF yafuata nyayo za FIFA
Kamati
ya Utendaji ya TFF, ambayo ilikuwa jijini Arusha kwaajili ya fainali ya
michuano ya Kombe la Shirikisho (ASFC), imefanya kongamano kubwa la
(TFF Executive Football Summit 2018) lililowakutanisha viongozi wa soka
kutoka mikoa 6 nchini.
Kongamano hilo lililoongozwa na Rais wa TFF Wallace Karia jana Juni 3, Mkoani Arusha, limejadili mambo mbalimbali ikiwemo kuboresha miundo mbinu ya michezo pamoja na vyama vya mikoa kuwekeza nguvu kwenye soka la vijana.
Wajumbe waliohudhuria 'TFF Executive Football Summit 2018', ni kutoka mikoa ya Singida, Dodoma, Manyara, Kilimanjaro, Tanga na wenyeji ambao ni Mkoa wa Arusha.
Mapema Mwaka huu FIFA ilifanya Kongamano kubwa kwa nchini wanachama zaidi ya 17 barani Africa na lilifanyika jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na Rais wa FIFA Gianni Infantino pamoja na Rais wa CAF Ahmed Ahmed.

No comments