Full-Width Version (true/false)


Tshishimbi alilia usajili Yanga

 


KIUNGO wa Yanga, Mkongo Papy Kabamba Tshishimbi, amekiangalia kikosi chao na namna wanavyocheza na kutoa ushauri juu ya kile kinachotakiwa kufanywa ili kuongeza makali kwenye timu hiyo. 

Tshishimbi alikuwa miongoni mwa wachezaji walioshuka dimbani wakati timu yake ikiondolewa kwenye michuano ya SportPesa Super Cup inayoendelea mjini hapa baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-1, kutoka kwa Kakamega Homeboyz. 

Akizungumza  mara baada ya mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Afraha, Nakuru, Tshishimbi, alisema timu inapaswa kufanya usajili wa maana kuongeza nguvu kwenye baadhi ya nafasi. 

"Tumepoteza mchezo katika hali ya kawaida tu na inatokea kwenye soka, lakini kukiimarisha kikosi chetu kwa ajili ya msimu ujao, ni lazima kusajili nguvu nyingine hasa katika nafasi ya kiungo na ushambuliaji," alisema Tshishimbi.

Aidha, alisema Yanga ina wachezaji wengi wazuri na wenye uwezo, lakini ni lazima kuongeza nguvu ili kutoa changamoto. "Nafikiri makocha wanafahamu zaidi nini cha kufanya, naamini msimu ujao tutakuwa kwenye nafasi nzuri na uwezo mkubwa wa kushindana," alisema. 

Yanga kwa sasa wapo kwenye mchakato wa usajili chini ya Mwenyekiti wa Mashindano, Hussein Nyika, kwa ajili ya kuiimarisha timu hiyo iliyotoka kapa msimu huu kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara na sasa ikiukosa ubingwa wa Kombe la SportPesa . 
Mashabiki waishia dakika 45Katika hatua nyingine mashabiki wa Yanga, juzi walijikuta wakiitazama timu yao kwa dakika 45 tu za kipindi cha kwanza kwenye mchezo dhidi ya Kakamega baada ya kuchelewa kuwasili mjini hapa wakitokea Dar es Salaam. 

Huku wakiamini kuwa wataendelea kuiangalia na kuishangilia timu yao kwenye michezo inayofuata, mashabiki hao waliokuja na basi la klabu hiyo walijikuta safari yao ikiishia kuitazama timu hiyo kwa dakika 45 za kipindi cha pili pekee

No comments

Powered by Blogger.