Full-Width Version (true/false)


“Tume ichunguze mgodi wa GGM”-Musukuma
Mbunge wa Geita vijijini (CCM) Joseph Musukuma, ameitaka Serikali kuunda tume ya kuchunguza mgodi wa dhahabu Geita (GGM) kwasababu uongozi wa mgodi huwa umekuwa ukinyanyasa wananchi hasa wachimbaji wadogowadogo wa madini. 

Musukuma amesema hayo leo Juni 1, 2018 Bungeni Jijini Dodoma, wakati wa kuchangia hoja mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi katika Wizira ya Madini na kuongeza kuwa uongozi wa mgodi umewafukuza wachimbaji wadogowadogo wenye leseni na ruhusa ya Mahakama mwaka 2016.

“Mheshimiwa Waziri (wa Madini) ukija hapa nataka utuambie kama GGM ni zaidi ya Serikali na ni zaidi ya muhimili wa majaji sita tuelewe, lakini kama sio sahihi basi ninaomba Mheshimiwa Waziri chukua hatua ya kuweza kusaidia watu hawa, mahakama imetoa hukumu ya kuwapa haki  wananchi hawa inatokeaje mtu mmoja tu GGM anatoa siku saba  kuwafukuza baada ya mbunge kuchangia hizi ni dharau” amesema Musukuma.

Mbunge huyo ameongeza kuwa Serikali ikae na viongozi wakiwemo madiwani ili kujua matatizo yanayotokana na mgodi wa GGM na kutaka serikali kuunda Tume kama zile za mchanga wa makinikia na madini ya Tanzanite.

Bunge kwasasa linajadili Bajeti ya Wizara ya madini katika mwaka wa fedha 2018/2019 na Waziri husika Angela Kairuki aliomba wabunge kuizinisha jumla ya shilingi bilioni 58.9 ambapo bilioni 19.6 zitatumika katika maendeleo na bilioni 39.2 kwaajili ya matumizi ya kawaida.

No comments

Powered by Blogger.