Full-Width Version (true/false)


"Tutaendelea kuwanyakua madereva"- Kamanda Muslim
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini Fortunatus Muslim amefunguka na wataendelea na zoezi lao la kunyakua magari barabarani yasiokidhi vigezo vinavyotakiwa kwa mujibu wa sheria kwa lengo la kutaka kunusuru ajali zisizokuwa na tija. 

Kamanda Muslim ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha East Africa Drive kilichorushwa hivi karibuni kutoka East Africa Radio baada ya kuwepo

"Kwa mujibu wa sheria chombo chochote cha moto kinapaswa kuingia barabarani kwa kuzingatia ubora wake na kufaa tembea barabarani kwa maana ya kwamba halitaweza kuleta au kusababisha athari kwa watumiaji wengine wa barabaranasio vinginevyo", amesema Kamanda Muslim.

Pamoja na hayo, Kamanda Muslim ameendelea kwa kusema "kitu kingine cha msingi hicho chombo cha moto lazima kiwe na bima kwa usalama wa mtumiaji na chombo chenyewe kwa hiyo hayo ni mambo ya msingi sana ya kuzingatia kwa mujibu wa sheria za usalama barabarani. Kwa hiyo tunaendelea kuwaonya madereva wote wafuate sheria na wale wasiotaka kufuata sisi tutaendelea kuwa nyakua kama anavyofanya 'mwewe na kipanga'.

No comments

Powered by Blogger.