Full-Width Version (true/false)


Ubora wa Lwandamina unavyoitesa Yanga

Klabu ya Yanga imekuwa kwenye mkwamo wa kupata ushindi tangu kuondoka kwa aliyekuwa kocha mkuu wa kikosi hicho George Lwandamina, ambapo katika mechi 13 ilizocheza bila Mzambia huyo imeshinda mechi moja tu.
Rekodi za Yanga ambayo inawakilisha nchi kwenye michuano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho barani Afrika, imepoteza mechi 8 kati ya 13 ilizocheza katika michuano yote na kufanya timu hiyo kuwa kwenye hali mbaya.

Katika mechi hizo 13 za Yanga, walinzi wake wameruhusu mabao 20 huku wao wakifunga mabao 7 pekee. Yanga pia imetoa sare kwenye mechi 4, na ushindi mmoja dhidi ya Mbao FC.

Zifuatazo ndio mechi na matokeo ya yake ambazo Yanga imecheza tangu Lwandamina arejee kwenye klabu yake ya zamani Zesco United ya nyumbani kwao Zambia.

Aprili 11, 2018; Yanga 1-1 Singida United (Ligi Kuu Dar es Salaam). Aprili 18, 2018; Welayta Dicha 1-0 Yanga SC (Kombe la Shirikisho). Aprili 22, 2018; Mbeya City 1-1 Yanga SC (Ligi Kuu Mbeya). Aprili 29, 2018; Simba 1 – 0 Yanga SC (Ligi Kuu Dar es Salaam). Mei 6, 2018; USM Alger 4-0 Yanga SC (Kombe la Shirikisho Algiers). Mei 10, 2018; Tanzania Prisons 2-0 Yanga SC (Ligi Kuu Mbeya). Mei 13; 2018; Mtibwa Sugar 1-0 Yanga SC (Ligi Kuu Morogoro).

Mei 16, 2018; Yanga SC 0-0 Rayon Sports (Kombe la Shirikisho Dar es Salaam). Mei 19, 2018; Yanga SC 0-1 Mwadui FC (Ligi Kuu Shinyanga). Mei 22, 2018; Yanga SC 1-0 Mbao FC (Ligi Kuu Dar es Salaam). Mei 25, 2018; Yanga SC 2-2 Ruvu Shooting (Ligi Kuu Dar es Salaam). Mei 28, 2018; Yanga SC 1-3 Azam FC (Ligi Kuu Dar es Salaam). Juni 3, 2018; Yanga SC 1-3 Kakamega Homeboys (SportPesa Super Cup).

No comments

Powered by Blogger.