Full-Width Version (true/false)


Ufuta umekuwa dili mkoani Lindi

MKUU wa mkoa wa Lindi,Godfrey Zambi amewaasa wakulima wa ufuta mkoani humu wasikubali kurubuniwa nakuuza kwa walañguzi.Kwasàbabu bei ya zao hilo msimu inaweza kuwa mzuri.

Zambi alitoa wito huo katika mtaa wa Mnazimmoja,manispaa ya Lindi alipotembelea ghala la kukusanyia mazao ya wakulima,ilikuona maendeleo ya ukusanyaji na maandalizi ya ununuzi wa zao hilo katika msimu huu.

Alisema wakulima wasikubali kulaghaiwa na kuwauzia walanguzi.Kwasababu kampuni zilizojitokeza kuomba kununua zao hilo ni nyingi nazinahitaji kiasi kingi kuliko kiasi  kilichozalishwa.Hivyo kunauwezekano mkubwa bei ya zao hilo kuwa kubwa.

Alibanisha kwamba hadi sasa kampuni 22 zimeomba kununua zao hilo.Ambazo zinahitaji kununua tani takribani 100,000.Huku makisio ya uzalishaji katika msimu huu yakiwa ni tani 45,000.


"Makisio yetu kwa msimu huu ni tani 45,000 tu.Wao wanataka jumla ya tani takribani 100,000 utaona kuwa mahitaji nimakubwa kuliko uzalishaji.Kwahiyo kunauwezakano mkubwa wa bei kuwa kubwa,"alisisitiza Zambi.

Mbali na kueleza hayo,amewataka viongozi na watendaji wa vyama vya msingi vya ushirika(AMCOS) kukagua ufuta unaokusanywa kutoka kwa wakulima,ili kuhakikisha kama hauchanganywi na mchanga au vitu vingine visivyohitajika.

Amewaonya pia wakulima wenye tabia yakuchanganya mazao na vitu visivyohitajika ili kuongeza uzito waache tabia hiyo.Kwasababu licha ya kuharibu soko la zao hilo,lakini nikosa.Hivyo atayekamatwa kwa kufanya hivyo atafikishwa kwenye vyombo vya sheria.Huku akiviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kufuatilia kwa karibu ununuzi na usafirishaji wa zao hilo.

Bei elekezi ya ufuta ambayo imetangazwa na serikali ya mkoa katika msimu huu  2018/2019 ni shilingi 1,750 kwa kila kilo moja.

No comments

Powered by Blogger.