Full-Width Version (true/false)


UHAI CUP kutimua vumbi Juni 9, Simba na Yanga ndani


Upangaji wa ratiba na makundi ya Ligi ya Vijana U20 kwa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara umefanyika leo Alhamis Juni 7,2018 Makao Makuu ya Azamtv.

Timu hizo 16 zimepangwa kwenye makundi manne yenye timu nne kila kundi.

Ligi hiyo inatarajia kuanza kutimua vumbi Juni 9,2018 mpaka Juni 21,2018 zikifanyika kwenye Jiji la Dodoma viwanja vya Chuo Kikuu cha Dodoma UDOM.

Kundi A
Young Africans 
Ruvu Shooting 
Mbeya City 
Mbao FC 

Kundi B
Simba 
Singida United 
Stand United
Njombe Mji 

Kundi C 
Azam FC 
Mtibwa Sugar 
Mwadui FC 
Majimaji FC 

Kundi D 
Tanzania Prisons 
Lipuli FC 
Kagera Sugar 
Ndanda FC

Katika kundi A Young Africans watafungua pazia la mashindano hayo dhidi ya Ruvu Shooting saa 8 mchana ikifuatiwa na mchezo wa pili Mbeya City dhidi ya Mbao FC Juni 9,2018 saa 10 jioni.

Mechi nyingine zitakazochezwa katika siku hiyo ya kwanza ni za kundi C ambapo Azam FC watacheza na Mtibwa Sugar saa 8 mchana ikifuatiwa na mchezo wa pili utakaoanza saa 10 kati ya Mwadui na Majimaji 

Kundi B wenyewe wataanza mechi zao Juni 10,2018 ambapo Simba watacheza dhidi ya Singida United nao Stand United watacheza na Njombe Mji saa 10 jioni.

Mechi nyingine za siku hiyo ni za Kundi D Tanzania Prisons dhidi ya Lipuli FC saa 8 mchana ikifuatiwa na mchezo wa Kagera Sugar dhidi ya Ndanda FC saa 10 jioni.

No comments

Powered by Blogger.